Amri
Waefeso 6:4
[4]Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Luka 17:1-4
[1]Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!
[2]Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
[3]Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.
[4]Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
TAFAKARI:
MUNGU hupenda kila mmoja wetu amuheshimu Kiumbe mwingine hata Kama umemzaa, heshima Ni lazima. Hata hivyo, Watoto nao Hawana KINGA ikiwa watawaadhibu wazazi wao kutokana na madhaifu waliyo nayo.
Comments
Post a Comment