Posts

Showing posts with the label Agano

KANISANI LEO.

Image
Yohana 14:1-12 [1]Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. [2]Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. [3]Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. [4]Nami niendako mwaijua njia. [5]Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? [6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. [7]Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. [8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. [9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? [10]Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. [11]Mnisadiki ya kwamba mimi...