Posts

Showing posts with the label Kanisa

SOMO LA MSINGI.

Image
Nehemia 2:17-20 [17]Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena. [18]Nikawaeleza habari ya mkono wa Mungu wangu ulivyokuwa mwema juu yangu; pia na maneno ya mfalme aliyoniambia. Nao wakasema, Haya! Na tuondoke tukajenge. Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema. [19]Lakini waliposikia Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Mtaasi ninyi juu ya mfalme? [20]Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu. TRANSLATION: Then I said to them, “You see the trouble we are in, t how Jerusalem lies in ruins with its gates burned. Come, let us build the wall of Jerusalem, that...

SOMO LA MSINGI.

Image
Yakobo 4:11-12 [11]Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu. [12]Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine? TRANSLATION: Speak not evil one of another, brethren. He that speaketh evil of his brother, and judgeth his brother, speaketh evil of the law, and judgeth the law: but if thou judge the law, thou art not a doer of the law, but a judge. James:4:11 There is one lawgiver, who is able to save and to destroy: who art thou that judgest another? James:4:12

SOMO LA MSINGI.

Image
Mathayo 16:24-25 [24]Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. [25]Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. Marko 15:21-22 [21]Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake. [22]Wakamleta mpaka mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa. Translation. Then said Jesus unto his disciples, If any man will come after me, let him deny himself, and take up his cross, and follow me. Matthew:16:24 For whosoever will save his life shall lose it: and whosoever will lose his life for my sake shall find it. Matthew:16:25 And they compel one Simon a Cyrenian, who passed by, coming out of the country, the father of Alexander and Rufus, to bear his cross. Mark:15:21 And they bring him unto the place Golgotha, which is, being interpreted, The place of a skull. Mark:1...

SOMO LA MSINGI.

Image
Mwanzo 18:1-15 [1]BWANA akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. [2]Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, [3]akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. [4]Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. [5]Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. [6]Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. [7]Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng’ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. [8]Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala. [9]Wakamwambia, Yu wapi Sara...

SOMO LA MSINGI.

Image
Maombolezo 3:19-21 [19]Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu,  Pakanga na nyongo. [20]Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo,  Nayo imeinama ndani yangu. [21]Najikumbusha neno hili,  Kwa hiyo nina matumaini. TAFSILI. Remembering mine affliction and my misery, the wormwood and the gall. Lamentations:3:19 My soul hath them still in remembrance, and is humbled in me. Lamentations:3:20 This I recall to my mind, therefore have I hope. Lamentations:3:21

KANISANI LEO.

Image
Yohana 14:1-12 [1]Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. [2]Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. [3]Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. [4]Nami niendako mwaijua njia. [5]Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? [6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. [7]Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. [8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. [9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? [10]Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. [11]Mnisadiki ya kwamba mimi...