Amri

Waefeso 6:4 [4]Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. Luka 17:1-4 [1]Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! [2]Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. [3]Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. [4]Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. TAFAKARI: MUNGU hupenda kila mmoja wetu amuheshimu Kiumbe mwingine hata Kama umemzaa, heshima Ni lazima. Hata hivyo, Watoto nao Hawana KINGA ikiwa watawaadhibu wazazi wao kutokana na madhaifu waliyo nayo.