Posts

Showing posts with the label Church

SOMO LA MSINGI.

Image
Ufunuo wa Yohana 3:14-22 [14]Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika;  Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. [15]Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. [16]Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. [17]Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. [18]Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. [19]Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. [20]Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. [21]Yeye ashinday...

SOMO LA MSINGI.

Image
Yakobo 4:11-12 [11]Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu. [12]Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine? TRANSLATION: Speak not evil one of another, brethren. He that speaketh evil of his brother, and judgeth his brother, speaketh evil of the law, and judgeth the law: but if thou judge the law, thou art not a doer of the law, but a judge. James:4:11 There is one lawgiver, who is able to save and to destroy: who art thou that judgest another? James:4:12

KANISANI LEO.

Image
Yohana 14:1-12 [1]Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. [2]Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. [3]Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. [4]Nami niendako mwaijua njia. [5]Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? [6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. [7]Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. [8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. [9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? [10]Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. [11]Mnisadiki ya kwamba mimi...