NENO LA LEO.
2 Wathesalonike 3:1-5
[1]Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;
[2]tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.
[3]Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.
[4]Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya.
[5]Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.
TAFAKARI:
Hakika Kazi ya kuhubiri injili Ni ngumu katika maisha ya Kibinadamu kwa sababu neno la MUNGU humteketeza Yule muovu ambaye kwa namna moja au nyingine huishi miongoni mwetu. Upo wakati shetani huja kwa umbo la Baba, Mama, Dada, Kaka na Wengine wengi Kisha hulenga kumjaribu huyo mtu aliye karibu na watu hawa.
Katika akili za Kawaida Ni ngumu kubishana na ndugu wa adamu au Watu wa Muhimu Kama Wazazi, ikitokea Hali Hiyo watu wengi huanguka katika mtego.
Washirika au waamini wote Hawana Budi kuwaombea wainjilisti na viongozi wote wa dini ili waweze kuishi ahadi za ubatizo na kupingana na Yule muovu kwa kuhubiri na kufundisha neno la MUNGU.
MUNGU amekwisha ahidi kuwa hatotuacha peke yetu katika Kazi zake yeye atakuwa nasi katika kusanyiko Mathayo 18:20.
Zaidi, MUNGU amehaidi kuwa hata waacha wamwaminio wajaribiwe kupita uwezo wao, 1Wakorintho 10:13.
Comments
Post a Comment