KUZALIWA KWA BWANA WETU YESU KRISTO.

Luka 2:10-12,14,16-17,20
[10]Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
[11]maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.
[12]Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.
[14]Atukuzwe Mungu juu mbinguni, 
Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.
[16]Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini.
[17]Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto.
[20]Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.

Luke 2:10,11,12,14,16-17,20
[10]And the angel said unto them, Fear not: for, behold, I bring you good tidings of great joy, which shall be to all people.
[11]For unto you is born this day in the city of David a Saviour, which is Christ the Lord.
[12]And this shall be a sign unto you; Ye shall find the babe wrapped in swaddling clothes, lying in a manger.
[14]Glory to God in the highest, and on earth peace, good will toward men.
[16]And they came with haste, and found Mary, and Joseph, and the babe lying in a manger.
[17]And when they had seen it, they made known abroad the saying which was told them concerning this child.
[20]And the shepherds returned, glorifying and praising God for all the things that they had heard and seen, as it was told unto them.

MAMBO MUHIMU KUHUSU HABARI HII. 
1. Yesu anapaswa kuzaliwa rohoni mwetu.
2. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni habari njema. 
3. Yesu anapozaliwa kwetu ni Utukufu kwa  Mungu na kwetu sisi tuliopo Duniani.
Tunapoazimisha kuzaliwa kwake tunatakiwa kuazimisha kwa kuonesha heshima kubwa kwa Mungu na upendo mkubwa Kati yetu. 
4. Kuzaliwa kwa Yesu huambatana na ishara. Tuendelee kumuomba Mungu atuwezeshe kuona Ishara za kuzaliwa kwake Rohoni mwetu. 
5. Ni lazima tushughulike na kuzaliwa kwa Yesu kwa Kutangaza uwepo wake. 
7.Ni lazima tumtukuze Mungu kwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo. 

Comments