KANISANI LEO.

Yohana 14:1-12
[1]Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
[2]Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
[3]Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
[4]Nami niendako mwaijua njia.
[5]Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
[7]Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
[8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
[9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
[10]Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.
[11]Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
[12]Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
TAFSIRI YA KIINGEREZA IPO CHINI (ENGLISH TRANSLATION IS AVAILABLE BELOW)
John 14:1-12
[1]Let not your heart be troubled: ye believe in God, believe also in me.
[2]In my Father's house are many mansions: if it were not so, I would have told you. I go to prepare a place for you.
[3]And if I go and prepare a place for you, I will come again, and receive you unto myself; that where I am, there ye may be also.
[4]And whither I go ye know, and the way ye know.
[5]Thomas saith unto him, Lord, we know not whither thou goest; and how can we know the way?
[6]Jesus saith unto him, I am the way, the truth, and the life: no man cometh unto the Father, but by me.
[7]If ye had known me, ye should have known my Father also: and from henceforth ye know him, and have seen him.
[8]Philip saith unto him, Lord, shew us the Father, and it sufficeth us.
[9]Jesus saith unto him, Have I been so long time with you, and yet hast thou not known me, Philip? he that hath seen me hath seen the Father; and how sayest thou then, Shew us the Father?
[10]Believest thou not that I am in the Father, and the Father in me? the words that I speak unto you I speak not of myself: but the Father that dwelleth in me, he doeth the works.
[11]Believe me that I am in the Father, and the Father in me: or else believe me for the very works' sake.
[12]Verily, verily, I say untoyou, He that believeth on me, the works that I do shall he do also; and greater works than these shall he do; because I go unto my Father.

Comments