SOMO LA MSINGI.

Mwanzo 45:1-24
[1]Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze.
[2]Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia.
[3]Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake.
[4]Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.
[5]Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.
[6]Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna.
[7]Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu.
[8]Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri.
[9]Fanyeni haraka, mmwendee baba yangu, mkamwambie, Hivi ndivyo asemavyo mwanao Yusufu, Mungu ameniweka kuwa bwana katika Misri yote, basi unishukie, usikawie.
[10]Nawe utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao, na wana wa wanao, na wanyama wako, ng’ombe zako, na yote uliyo nayo. Nami nitakulisha huko;
[11]maana bado imesalia miaka mitano ya njaa; usije ukaingia katika uhitaji, wewe, na nyumba yako, na yote uliyo nayo.
[12]Na tazama, macho yenu yanaona, na macho ya ndugu yangu Benyamini, ya kwamba ni kinywa changu mimi kinachosema nanyi.
[13]Nanyi mtamwarifu baba yangu habari za fahari yangu yote katika Misri, na za vyote mlivyoviona; mkafanye haraka kumleta huku baba yangu.
[14]Akaanguka shingoni mwa ndugu yake Benyamini, akalia; Benyamini naye akalia shingoni mwake.
[15]Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze wakazungumza naye
[16]Habari ikasikika nyumbani mwa Farao kusema, Ndugu zake Yusufu wamekuja. Ikawa vema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake.
[17]Farao akamwambia Yusufu, Uwaambie ndugu zako, Fanyeni hivi; wachukuzeni mizigo wanyama wenu, mwondoke mwende nchi ya Kanaani;
[18]kisha mkamtwae baba yenu, na watu wa nyumbani mwenu, mkanijie; nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.
[19]Nawe umeamriwa; fanyeni hivi, mjitwalie magari katika nchi ya Misri kwa watoto wenu wadogo na wake zenu, mkamchukue baba yenu mje.
[20]Wala msivisumbukie vyombo vyenu, maana mema ya nchi yote ya Misri ni yenu.
[21]Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. Yusufu akawapa magari kama Farao alivyoamuru, akawapa na chakula cha njiani.
[22]Akawapa kila mtu nguo za kubadili; lakini Benyamini, alimpa fedha mia tatu na mavazi matano ya kubadili.
[23]Na babaye akampelekea kama hivi, punda kumi waliochukua mema ya Misri, na punda wake kumi waliochukua nafaka, na mikate, na chakula kwa babaye njiani.
[24]Akaagana na ndugu zake, wakaenda zao; naye akawaambia, Msigombane njiani.

TRANSLATION.

Then Joseph could not p


control himself before all those who stood by him. He cried, “Make everyone go out from me.” So no one stayed with him when Joseph made himself known to his brothers. 2#And he wept aloud, so that the Egyptians heard it, and the household of Pharaoh heard it. 3#And Joseph said to his brothers, q “I am Joseph! Is my father still alive?” But his brothers could not answer him, for they were dismayed at his presence.
4#So Joseph said to his brothers, “Come near to me, please.” And they came near. And he said, “I am your brother, Joseph, r whom you sold into Egypt. 5#And now do not be distressed or angry with yourselves because you sold me here, s for God sent me before you to preserve life. 6#For the famine has been in the land these two years, and there are t yet five years in which there will be neither u plowing nor harvest. 7#And God sent me before you to preserve for you a remnant on earth, and to keep alive for you many survivors. 8#So it was not you who sent me here, but God. He has made me a father to Pharaoh, and lord of all his house and v ruler over all the land of Egypt. 9#Hurry and go up to my father and say to him, ‘Thus says your son Joseph, God has made me lord of all Egypt. Come down to me; do not tarry. 10#w You shall dwell in the land of Goshen, and you shall be near me, you and your children and your children's children, and your flocks, your herds, and all that you have. 11#x There I will provide for you, for there are yet five years of famine to come, so that you and your household, and all that you have, do not come to poverty.’ 12#And now your eyes see, and the eyes of my brother Benjamin see, that it is y my mouth that speaks to you. 13#You must tell my father of all my honor in Egypt, and of all that you have seen. Hurry and z bring my father down here.” 14#Then he fell upon his brother Benjamin's neck and wept, and Benjamin wept upon his neck. 15#And he kissed all his brothers and wept upon them. After that his brothers talked with him.
16#When the report was heard in Pharaoh's house, “Joseph's brothers have come,” it pleased Pharaoh and his servants. 17#And Pharaoh said to Joseph, “Say to your brothers, ‘Do this: load your beasts and go back to the land of Canaan, 18#and take your father and your households, and come to me, and a I will give you the best of the land of Egypt, and you shall eat the fat of the land.’ 19#And you, Joseph, are commanded to say, ‘Do this: take b wagons from the land of Egypt for your little ones and for your wives, and bring your father, and come. 20#Have no concern for 1 your goods, for the best of all the land of Egypt is yours.’”
21#The sons of Israel did so: and Joseph gave them b wagons, according to the command of Pharaoh, and gave them provisions for the journey. 22#To each and all of them he gave c a change of clothes, but to Benjamin he gave three hundred shekels 2 of silver and d five changes of clothes. 23#To his father he sent as follows: ten donkeys loaded with the good things of Egypt, and ten female donkeys loaded with grain, bread, and provision for his father on the journey. 24#Then he sent his brothers away, and as they departed, he said to them, e “Do not quarrel on the way.”


Comments