SOMO LA MSINGI
Yakobo 2:17-26
[17]Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
Even so faith, if it hath not works, is dead, being alone.
[18]Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
Yea, a man may say, Thou hast faith, and I have works: shew me thy faith without thy works, and I will shew thee my faith by my works.
[19]Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
Thou believest that there is one God; thou doest well: the devils also believe, and tremble.
[20]Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
But wilt thou know, O vain man, that faith without works is dead?
[21]Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
Was not Abraham our father justified by works, when he had offered Isaac his son upon the altar?
[22]Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
Seest thou how faith wrought with his works, and by works was faith made perfect?
[23]Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
And the scripture was fulfilled which saith, Abraham believed God, and it was imputed unto him for righteousness: and he was called the Friend of God.
[24]Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
Ye see then how that by works a man is justified, and not by faith only.
[25]Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
Likewise also was not Rahab the harlot justified by works, when she had received the messengers, and had sent them out another way?
[26]Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
For as the body without the spirit is dead, so faith without works is dead also.
Comments
Post a Comment