SOMO LA MSINGI.

TUENDELEE KUZIKATAA NJIA ZA KIPAGANI.

MHUBIRI: FAUSTINE GUTAPAKA.
Waefeso 5:3-20
[3]Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; 
But fornication, and all uncleanness, or covetousness, let it not be once named among you, as becometh saints;
[4]wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. 
Neither filthiness, nor foolish talking, nor jesting, which are not convenient: but rather giving of thanks.
[5]Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 
For this ye know, that no whoremonger, nor unclean person, nor covetous man, who is an idolater, hath any inheritance in the kingdom of Christ and of God.
[6]Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. 
Let no man deceive you with vain words: for because of these things cometh the wrath of God upon the children of disobedience.
[7]Basi msishirikiane nao. 
Be not ye therefore partakers with them.
[8]Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru, 
For ye were sometimes darkness, but now are ye light in the Lord: walk as children of light:
[9]kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; 
(For the fruit of the Spirit is in all goodness and righteousness and truth;)
[10]mkihakiki ni nini impendezayo Bwana. 
Proving what is acceptable unto the Lord.
[11]Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; 
And have no fellowship with the unfruitful works of darkness, but rather reprove them.
[12]kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena. 
For it is a shame even to speak of those things which are done of them in secret.
[13]Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru. 
But all things that are reproved are made manifest by the light: for whatsoever doth make manifest is light.
[14]Hivyo husema, 
Amka, wewe usinziaye, 
Ufufuke katika wafu, 
Na Kristo atakuangaza. 
Wherefore he saith, Awake thou that sleepest, and arise from the dead, and Christ shall give thee light.
[15]Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 
See then that ye walk circumspectly, not as fools, but as wise,
[16]mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 
Redeeming the time, because the days are evil.
[17]Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. 
Wherefore be ye not unwise, but understanding what the will of the Lord is.
[18]Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; 
And be not drunk with wine, wherein is excess; but be filled with the Spirit;
[19]mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; 
Speaking to yourselves in psalms and hymns and spiritual songs, singing and making melody in your heart to the Lord;
[20]na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; 
Giving thanks always for all things unto God and the Father in the name of our Lord Jesus Christ;

Comments