ATUKUZWE MUNGU.
ATUKUZWE MUNGU.
FAUSTINE GUTAPAKA.
Waefeso 1:3-14
[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Blessed be the God and Father of our Lord Jesus Christ, who hath blessed us with all spiritual blessings in heavenly places in Christ:
[4]kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
According as he hath chosen us in him before the foundation of the world, that we should be holy and without blame before him in love:
[5]Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
Having predestinated us unto the adoption of children by Jesus Christ to himself, according to the good pleasure of his will,
[6]Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
To the praise of the glory of his grace, wherein he hath made us accepted in the beloved.
[7]Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
In whom we have redemption through his blood, the forgiveness of sins, according to the riches of his grace;
[8]Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;
Wherein he hath abounded toward us in all wisdom and prudence;
[9]akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo.
Having made known unto us the mystery of his will, according to his good pleasure which he hath purposed in himself:
[10]Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;
That in the dispensation of the fulness of times he might gather together in one all things in Christ, both which are in heaven, and which are on earth; even in him:
[11]na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
In whom also we have obtained an inheritance, being predestinated according to the purpose of him who worketh all things after the counsel of his own will:
[12]Nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo tumaini letu.
That we should be to the praise of his glory, who first trusted in Christ.
[13]Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
In whom ye also trusted, after that ye heard the word of truth, the gospel of your salvation: in whom also after that ye believed, ye were sealed with that holy Spirit of promise,
[14]Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.
Which is the earnest of our inheritance until the redemption of the purchased possession, unto the praise of his glory.
Comments
Post a Comment