YACHUNGUZE MAWAZO YAKO KAMA YANA MADHARA.

YACHUNGUZE MAWAZO YAKO KAMA YANA MADHARA.

MHUBIRI: EV. YOTHAM FILIMON (TENDAWEMA)

Neno la Mungu linazungumza habari ya mke na mume na kwa kawaida wanafamilia wa aina hiyo lazima wawe na mipango.
Kwa wakati ule Kanisa la Yerusalemu liliazimia kuchangia na kusaidia watu wasiojiweza. Katika jambo hilo kila Mkristo aliweza kujitoa kitu alichoweza. Katika Matendo ya Mitume 4:36 anaonekana Yusufu mtu wa Kipro aliuza shamba na fedha iliyopatikana akaiweka chini ya miguu ya mitume.
Jambo la kushangaza Anania na mkewe Safira walifanikiwa kuuza shamba lao lakini baada ya kupata fedha waliiingia tamaa na kuanza kuwaza kwenda kinyume na makubaliano ya KANISA. Walipoenda mbele za Mitume wakapanga kusema uongo kuhusu kiasi walichopata baada ya kuuza shamba. Kwa sababu walishawaza mawazo mabaya bila kujua madhara yake. Petro akiwa katika Roho Mtakatifu anamuuliza Anania na Anania anasema uongo na kwa dhambi hiyo anakufa hapohapo. Mke wake naye bila kujua alipoulizwa alisema uongo naye akafa na kuzikwa jirani na mume wake.
Hakuna kitu kilicho mali yetu. Kila mali ni mali ya Mungu na akiamua kuichukua anaichukua bila shida na inapotea.
Matendo ya Mitume 5:6-11
[6]Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. 
And the young men arose, wound him up, and carried him out, and buried him.
[7]Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. 
And it was about the space of three hours after, when his wife, not knowing what was done, came in.
[8]Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. 
And Peter answered unto her, Tell me whether ye sold the land for so much? And she said, Yea, for so much.
[9]Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. 
Then Peter said unto her, How is it that ye have agreed together to tempt the Spirit of the Lord? behold, the feet of them which have buried thy husband are at the door, and shall carry thee out.
[10]Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. 
Then fell she down straightway at his feet, and yielded up the ghost: and the young men came in, and found her dead, and, carrying her forth, buried her by her husband.
[11]Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya. 
And great fear came upon all the church, and upon as many as heard these things.

Comments