SISI TULIO NA NGUVU.

SISI TULIO NA NGUVU.

MHUBIRI: OPTATUS GERSHON.
Warumi 15:1-3
[1]Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. 
We then that are strong ought to bear the infirmities of the weak, and not to please ourselves.
[2]Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe. 
Let every one of us please his neighbour for his good to edification.
[3]Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi. 
For even Christ pleased not himself; but, as it is written, The reproaches of them that reproached thee fell on me.

Walio na Nguvu ni akina nani?
Ni wale waliojawa na Roho Mtakatifu. 
Hata hivyo, Nguvu zetu hudhihirishwa tujaribiwapo. 
Kila mmoja Kanisani ana Nguvu zake na Nguvu hizo hutegemea sana kiasi cha Imani alicho nacho mtu husika.
Ni vizuri kuepuka kujipenda bali tuwapendeze jirani zetu. Maana hawa majirani ndio mabarozi wetu. 
Labda niulize. Jirani ni nani?
Jirani mtu yeyote aliye karibu yako. Inawezekana uko nae sokoni, kazini, nyumbani kwako au shambani.
Jirani ni mtu ambaye anaweza kutoa msaada wakati wa uhitaji, ukizingatia kwamba watu wengi huishi mbali na ndugu zao.
Watu wengi wamepumbazwa na fedha lakini ukweli ni mwamba fedha hawezi kutatua kila kitu. Mtu anaweza kuzidiwa usiku pamoja na fedha alizonazo anaweza kushindwa hata kunyanyua simu lakini jirani akisikia yowe au kelele zisizo za kawaida atakimbia haraka kuuliza na kutoa msaada.
Mtu yeyote atahesabika kuwa anamwabudu Mungu kwa kupitia namna anavyoishi vizuri na watu wake wa karibu.
Kwa mfano. Hezekia alipougua karibu ya kufa alimuomba Mungu kwa kumkumbusha mema aliyotenda maishani mwake, 2Wafalme 20:1-6
Hata hivyo, mfuga mbwa hupenda mbwa mtulivu. Mbwa mzurulaji na mharifu lazima auawe ama na watu wa nje au mfugaji mwenyewe. Ndivyo na Mungu alivyo. Mungu akiona mtu amekuwa msumbufu na mdhambi kwa binadamu wenzake anamvuna ili watu waishi kwa amani.


Comments