KUJITENGA NA UONGO
TUKATAE KUSEMA UONGO.
MHUBIRI: WINFRIDA JONATHAN
Utangulizi.
Mithali 14:25b.Maana ya uongo ni udanganyifu. Yaani kinyume cha Ukweli. Hata hivyo, Biblia inaonya mengi kuhusu uongo, kutoka 5:20, Kutoka 20:16.
Tusifanye wangine wateseke kwa sababu ya uongo. Kutoka 23:1a, Usivumishe habari za uongo. Maandiko yanakataa tabia ya kusambaza uongo.
Kutoka 23:7a, jitenge mbali na neno uongo. Pale unapoona uongo unaweza kufanyika tafuta namna ya kukaa mbali na mazingira hayo. Lazima tuwe tofauti na watu wa mtaifa.
Mambo ya Walawi 19:12a, msiape uongo kwa Jina Langu. Kwa mfano mtu anadanganya halafu anasema Haki ya Mungu, huko ni kumdhihaki Mungu.
Madhara ya uongo.
Zab 31:6, Nawachukia wao washikao yasiyofaa ya uongo. Zab 31:18, midomo ya uongo iwe na ububu. Maana yake ni kufungwa kinywa na Mungu atafanya hilo.
Mithali 19:5, Shahidi wa uongo hakosi, ataadhibiwa. Hakika maandiko yanasema mtu kama hiyo hataokoka. Mithali 19:9 inasisitiza kuhusu kuangamia kwa mtu wa uongo.
Kwa hiyo, tuendelee kumtumikia Mungu tukiukataa uongo, tusiseme uongo kwa watoto ili wasizozee uongo.
USHAURI WA MUNGU.
Mithali 12:22, Midomo ya Uongo ni chukizo kwa Mungu bali Mungu huwafurahia waaminifu.
Comments
Post a Comment