NIAMBIE ASILI YA NGUVU ZAKO.

NIAMBIE ASILI YA NGUVU ZAKO.

MHUBIRI: MCH. JONATHAN BUCHA.

Waamuzi 16:15-22
Samson ni mtoto wa mtu mmoja aliyeitwa Manoa na  wake hakutajwa. Mke wa Manoa alikuwa tasa. 
Malaika wa Bwana aliwatokea na kusema watapata mtoto naye huyo mtoto asije akanyolewa nywele naye wazazi wake wasiwe najisi wala kutumia mvinyo.

Samson alitengwa na Mungu kuwa mtumishi wake, ndivyo ilivyo kwetu sote. Samson anachaguliwa wakati ambao Israel haina mfalme bali Waamuzi. Kwa hiyo Samson alisimama baada ya Waamuzi wengine kupita. 

Wafilist ni miongoni mwa mataifa yaliyopigana vita muda mrefu na Israel. Samson anainuliwa wakati ambao wana wa Israel wako katika mateso makali na yeye aliinuliwa kama mkombozi wao.

Delila alikuwa mwanamke wa kifilisti aliyekuwa kahaba na kupendwa na Samson ( Nafikiri ni mpango wa Mungu) japokuwa Delila hakuwa na ushuda mzuri. Samson alimpenda sana Delila bila kujali kuwa anatoka katika maadui zake. Kwa sababu hiyo, Delila alifanyika mtego kwa Samson. 

Mungu alimpa NGUVU nyingi sana Samson tofauti na binadamu wengine ili kuwakomboa wana wa Israeli. Kwa kuwa Nguvu za Samson zilikuwa katika Nywele zake zilizokuwa na vichungi saba (07). Mungu alikataza zisinyolewe kamwe ili asiwe dhaifu. Kwa sababu hiyo, Samson aliwatetea sana wana wa Israel na kuua wafilisti wengi sana.



Tabia ya Samson kama ilivyo kwa wanaume wengine, alipenda wanawake. Maamuzi ya Samson kumpenda Delila na kusema siri yake in kosa kwa MUNGU, naye Mungu alimuacha. Hivyo, kwa sababu ya upendo kwa Delila Samson alifichua siri baada ya kusumbuliwa mara tatu na mkewe.

Katika maisha yetu tunatakiwa tumbainishe Delila anaetusonga na kutufanya tusiwe waaminifu mbele za Mungu.

Waamuzi 16:15-22
[15]Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. 
And she said unto him, How canst thou say, I love thee, when thine heart is not with me? thou hast mocked me these three times, and hast not told me wherein thy great strength lieth.
[16]Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. 
And it came to pass, when she pressed him daily with her words, and urged him, so that his soul was vexed unto death;
[17]Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. 
That he told her all his heart, and said unto her, There hath not come a razor upon mine head; for I have been a Nazarite unto God from my mother's womb: if I be shaven, then my strength will go from me, and I shall become weak, and be like any other man.
[18]Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao. 
And when Delilah saw that he had told her all his heart, she sent and called for the lords of the Philistines, saying, Come up this once, for he hath shewed me all his heart. Then the lords of the Philistines came up unto her, and brought money in their hand.
[19]Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. 
And she made him sleep upon her knees; and she called for a man, and she caused him to shave off the seven locks of his head; and she began to afflict him, and his strength went from him.
[20]Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha. 
And she said, The Philistines be upon thee, Samson. And he awoke out of his sleep, and said, I will go out as at other times before, and shake myself. And he wist not that the LORD was departed from him.
[21]Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza. 
But the Philistines took him, and put out his eyes, and brought him down to Gaza, and bound him with fetters of brass; and he did grind in the prison house.
[22]Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake. 
Howbeit the hair of his head began to grow again after he was shaven.


Comments