WEMA KAMILI.

WEMA KAMILI.

MHUBIRI: MCH.  JONATHAN BUCHA.
Maneno ambayo Yesu Kristo anawaambia mafarisayo na Masadukayo. 
Watu hawa walijifanya wachamungu wakienda hata katika njiapanda kufundisha neno la Mungu. Yesu anawatahadharisha watu kuwa makini na chachu yao kwa sababu wanajionesha kuwa ni watu wa kumcha Mungu lakini sivyo, wanafiki wakubwa. Yesu anasema watu kama hawa hawapati thawabu machoni pa Mungu.
MTU anaweza kujionesha ni mpole na huwezi kutambua chuki kwa macho ya kawaida lakini ni mfitini na mgombanishi, msengenyaji n.k
Nitolee mfano akina mama wa kisukuma, wao wamefundishwa kuheshimu mume na wanaowazidi umri. Hata baadhi ya waha wanaheshima nzuri lakini wengi wanaigiza. 
Baadhi ya wanawake wa kiha wanaheshima ya kujionesha kwa watu lakini kwa waume zao hawayafanyi hayo ya heshima. 

Hiyo ni heshima ya kinafiki. Kila mmoja atende wema kutoka moyoni, kwa Mungu na kwa watu wote. Wapo baadhi ya watu wanajinyenyekeza ili kupata kitu. Baada ya kupata kitu kwa heri mwalimu(hawanyenyekei tena).

Watu walijificha wakati wa kuchumbiana lakini baada ya kuolewa ndoa imekuwa vita, hawaelewani. Kuna baadhi ya watu hata ukimtembelea hawezi kukupa kiti ukae na hata akikupa kiti lengo wengine wamwone mwema lakini hana wema maana anaweza asikupe chakula au kinywaji.

Wakati wa zamani binti alikuwa hachumbiwi njiani lakini sasa kabla ya binti kuolewa ameshafika nyumbani kwa kijana. Mimi binti akifika nyumbani kwangu akifuata kijana wangu, nitamwambia kijana wangu hafai huyo, maana amejileta mwenyewe.
Zamani, binti akikupenda ukamwambia nakuja kwenu atakupokea hajifichi, na wakati wa kuondoka atakusindikiza. Kinyume na hapo alikuwa hapendi huyo mchumba.

Kuna mkristo anaabudu  Kanisani vizuri lakini lengo aonekane na watu, kwenda kwa waganga, umbea n.k bado anavyo kila Siku huo sio wema. Wakristo wengine wamekuwa kikwazo kwa wengine kumjua Yesu Kristo(Kuokoka)

Matthew 6:1
[1]"Beware of practicing your righteousness before men to be noticed by them; otherwise you have no reward with your Father who is in heaven.



Comments