WENYE UKOMA 10.
WENYE UKOMA 10.
MHUBIRI: MCH. JONATHAN BUCHA.
Luka 17:11-17
Sisi kama wakoma kumi.
Maana ya UKOMA ni dhambi. Tumrudie Mungu kama yule mmoja kati ya kumi. Tisa hawakumkumbuka Mungu baada ya kufanikiwa. Tunapomkumbuka Mungu naye atatupokea. Hii humaanisha kuwa katika Mafanikio tuwe na shukrani tumkumbuke Mungu aliye tupa uhai tusimsahau.Amina .
[11]Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.
And it came to pass, as he went to Jerusalem, that he passed through the midst of Samaria and Galilee.
[12]Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
And as he entered into a certain village, there met him ten men that were lepers, which stood afar off:
[13]wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
And they lifted up their voices, and said, Jesus, Master, have mercy on us.
[14]Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
And when he saw them, he said unto them, Go shew yourselves unto the priests. And it came to pass, that, as they went, they were cleansed.
[15]Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
And one of them, when he saw that he was healed, turned back, and with a loud voice glorified God,
[16]akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
And fell down on his face at his feet, giving him thanks: and he was a Samaritan.
[17]Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
And Jesus answering said, Were there not ten cleansed? but where are the nine?
Comments
Post a Comment